IQNA

Vikao vya Qur'ani kufanyika mjini London mwezi wa Ramadhani

23:50 - July 16, 2012
Habari ID: 2370145
Vikao maalumu vya Qur'ani ambavyo vimepangwa kufanyika katika mwezi wa Ramadhani chini ya anwani ya 'Kutafakari kwenye Qur'ani; Njia ya Maisha' vitafanyika katika Kituo cha Kiislamu mjini London Uingereza.
Kwa mujibu wa kituo hicho, vikao hivyo vitafanyika katika fremu ya tamasha la nane la kiutamaduni la Ramadhani ambalo litajumuisha ratiba nyingine ikiwa ni pamoja na usomaji wa dua, usimamishaji wa swala za jamaa za Maghrib na Isha pamoja na kutolewa futari.
Kituo cha Kiislamu cha London kimewapongeza Waislamu wote duniani kwa mnasaba wa kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani na kusema kuwa kituo hicho kitaawalika wanazuoni na wasomi mbalimbali wa Kiislamu ambao watatoa mafunzo na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusiana na Qur'ani na vilevile sababu za kuteremshwa aya zake.
Kituo hicho pia kitakuwa na vikao tofauti vya kutoa mafunzo ya kusoma Qur'ani katika siku za mwezi mtukufu wa Ramdhani ambavyo vitakuwa vikianza kabla ya swala za Magharibi na Isha. 1054117
captcha