Masomo hayo yatatolewa na Hujjatul Islam Harasaniyan. Wakati na sehemu ya kufanyika masomo hayo itatangazwa baadaye na idara ya masomo na utafiti ya kituo hicho.
Huku kikiwapongeza Waislamu kwa mnasaba wa kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani kituo hicho kimesema kuwa vikao vya Qur'ani maalumu kwa wanaume vitakuwa vikifanyika masaa mawili baada ya swala za jamaa za Adhuhuri na Alasiri na vya wanawake masaa mawili kabla ya swala za Magharibi na Isha katika mwezi huo mtukufu.
Swala za jamaa zitakuwa zikiongozwa na Hujjatul Islam wal Muslimeen Taqawiyan na kisha dua ya Iftitaah kuongozwa na Haj Muhsin Sheikh Zeinu ad-Deen. Kujibu maswali ya kisheria na kifikihi ni sehemu nyingine ya ratiba maalumu za mwezi mtukufu wa Ramadhani zitakazotekelezwa katika kituo hicho.
Ratiba za daku ambazo zinajumuisha usomaji Qur'ani na dua zitakuwa zikianza saa moja kabla ya daku. Ratiba za futari zitajumuisha usomaji Qur'ani, dua, mawaidha swala za Magharibi na Isha, futari na kisha dua ya Iftitaah.
Maombolezo ya kifo cha Bibi Fatma (as) katika usiku wa kuamkia tarehe 10 Ramadhani, sherehe za kuzaliwa Imam Hassan Mujtaba (as) nusu ya mwezi huo na swala za jamaa pamoja na swala ya Idul Fitr ni sehemu za ratiba za kituo hicho cha Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Marasimu maalumu ya usiku wa Leilatul Qadr katika tarehe 19, 21 na 23 pia yatahuishwa katika kituo hicho. 1054186