IQNA

Tovuti ya Qur'ani Tukufu yazinduliwa Uturuki

23:46 - July 16, 2012
Habari ID: 2370149
Taasisi ya Masuala ya Kidini ya Uturuki limezindua Tovuti ya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya kutumiwa na Waislamu wa nchi hiyo wanaojishughulisha na masuala ya tarjumi ya Qur'ani kwa lugha ya Kituruki.
Tovuti hiyo ina vitengo mbalimbali kama vile orodha ya sura, maonyesho ya aya na sura kwa lugha ya Kiarabu, tarjumi na tafsiri za sura kwa lugha ya Kituruki sambamba na sauti, kitafutia maneneo na maktaba.
Hiyo ndiyo tovuti kubwa zaidi ya Qur'ani ambayo imeandaliwa na taasisi iliyotajwa nchini Uturuki kwa ajili ya kusoma na kujifunza Qur'ani Tukufu. Kwa kadiri kwamba kila mtu anayetumia tovuti hiyo anaweza kujifunza Qur'ani Tukufu na kutamka vizuri maneno yake, jinsi ya kuswali na kusoma dua baada ya kupitia vikao na hatua 18 katika tovuti hiyo.
Tovuti inayozungumziwa ilizinduliwa rasmi siku ya Jumamosi. 1054624
captcha