IQNA

Nakala ya kwanza ya Qur'ani zenye hati ya braille yazinduliwa Yemen

21:20 - July 17, 2012
Habari ID: 2371222
Nakala ya kwanza kabisa ya Qur'ani zenye hati ya braille kwa ajili ya walemavu wa macho imezinduliwa nchini Yemen.
Sherehe ya uzinduzi wa nakala hiyo ya Qur'ani ya walemavu wa macho imesimamiwa na jumuiya ya Aman inayojishughulisha na masuala ya walemavu hao.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Yemen Ahmad Abiid ameipongeza jumuiya ya Aman na kusema iliasisiwa mwaka 1990 na hadi sasa imefanya kazi kubwa katika kuwasaidia walemavu wa macho nchini Yemen ikiwa ni pamoja na kuchapisha nakala za Qur'ani kwa hati ya braille.
Vilevile Waziri wa Wakfu na Miongozo wa Yemen Hamoud Abbad amesema katika sherehe hiyo kwamba wizara yake itachapicha nakala nyingi za Qur'ani hiyo na kwamba inawaswaidia na kuwahami walemavu wa macho.
Kwa upande wake Mkuu wa jumuiya ya Aman amesema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Qur'ani yenye hati ya braille kuzinduliwa nchini Yemen. Amesema nakala 150 za Qur'ani hiyo zitakuwa zikichapisha kila mwaka nchini Yemen kwa ajili ya walemavu wa macho. 1055344
captcha