IQNA

Iran kuandaa Olimpiadi ya Qur’ani katika nchi 40 duniani

15:26 - July 18, 2012
Habari ID: 2371776
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa chenye makao yake katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran kimetangaza mpango wa kuandaa Olimpiadi ya Kimataifa ya Qur’ani na Hadithi katika zaidi ya nchi 40 duniani.
Akizungumza na IQNA, Hussein Assadi Mkuu wa Kituo cha Qur’an na Itrat katika chuo hicho amesema tayari kituo hicho kimeshaandaa vikao kadhaa vya Qur’ani na kidini kote duniani.
Ameongeza kuwa Olimpiadi hiyo itakuwa na vitengo 92. Amesema vitengo hivyo ni kama vile kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu, kuhifadhi Nahjul Balagha, Sahifa Sajjadiyya, tafsiri na ufahamu wa Qur’ani, sayansi za Qur’ani, falsafa ya Hija, tarjumi ya Qur’ani, uandishi wa insha nk.
‘Wanachuo 17000 tayari wameshasajilisha majina yao na hili linaashiria ongezeko kubwa la washiriki ikilinganishwa na Olimpiadi iliyopita,’ amesema.
Mkuu wa Kituo cha Qur’an na Itrat katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa amesema sherehe za kufunga Olimpiadi hiyo zitafanyika katika mkesha wa Maulidi ya Mtume SAW mwakani.
1055686
captcha