IQNA

Qur'ani inayonasibishwa kwa Imam Ali (as) yaonyeshwa kwenye kibanda cha Uturuki mjini Tehran

13:58 - July 19, 2012
Habari ID: 2372531
Qur'ani Tukufu ambayo inasemekana kuwa iliandikwa kwa mkono wa Imam Ali (as) inaonyeshwa katika kibanda cha shirika la uchapishaji la Hizmet la nchini Uturuki katika maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea mjini Tehran.
Nuskha nyingine ya Qur'ani inayosemekana imeandikwa na Othman bin Affan ni miongoni mwa vitabu muhimu vya kihistoria vinavyoonyeshwa kwenye kibanda hicho. Licha ya kuwa hadi sasa kitengo cha vibanda vya kimataifa katika maonyesho hayo hakijafunguliwa rasmi, lakini kibanda hicho kimepokea wageni wengi kadiri kwamba wasisimamizi wa maonyesho hayo wamewaruhusu watembelee kibanda hicho na pia kingine cha Lebanon. 1056917
captcha