IQNA

Mbinu mpya ya kuhifadhi Qur’ani yawasilishwa Iran

11:23 - July 20, 2012
Habari ID: 2372573
Mbinu ya kisasa kabisa za kuhifadhi Qur’ani Tukufu imewasilishwa katika maonyesho ya 20 kimataifa ya Qur’ani Tukufu Tehran.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mbinu hiyo ya kuhifadhi Qur’ani kwa njia ya simu imearifishwa na Kituo cha Darul Qur’an cha ‘Nyumba ya Leba’ Iran. Kwa mujibu wa mbinu hiyo mshiriki anaweza kuhifadhi Qur’ani nzima kwa muda wa miaka miwili, mitatu au minne.
Mbinu hii ni muafaka hasa kwa wale ambao hawawezi kufika binafsi katika chuo cha Qur’ani. Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu Tehran mwaka huu yanalenga maudhui kadhaa Qur’ani Tukufu kama vile familia, sayansi za jamii, mwamko wa Kiislamu, wenye kusilimu na vyuo vya kidini.
Mbali na Iran nchi zingine zonazoshiriki katika maonyesho hayo ni India, Pakistan, Bahrain, Albania, Uturuki, Thailand, Iraq, Myanmar, Syria, Afghanistan, Bosnia na Herzegovina na Sri Lanka. Maonyesho hayo ambayo hufanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani yataendelea hadi Agosti 14.
1055709
captcha