IQNA

Mashindano makubwa ya Qur'ani kufanyika Tanzania

14:39 - July 21, 2012
Habari ID: 2373698
Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania kikishirikiana na Waislamu wa nchi hiyo kimepanga kuandaa mashindano kadhaa makubwa ya Qur'ani Tukufu yatakayowashirikisha Waislamu wote wa Kishia na Kisuni kwa mnasaba wa kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Baadhi ya mashindano hayo ni yale yanayotazamiwa kuandaliwa kwa ushirikiano wa jumuiya ya shule za sekondari ya mjini Dar es Salaam, mashindano ya Qur'ani katika Msikiti wa Idriss na mashindano ya Qur'ani kupitia Redio Kheir ya mjini Dar es Salaam. Kitengo hicho cha utamaduni pia kimepanga kuwa kitaandaa mashindano mengine ya Qur'ani kieneo kwa ushirikiano wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, Taasisi ya Kiislamu ya Istiqama na Jumuiya ya Mashia wa Khoja Ithna Asheri.
Mashindano mengine kama hayo yamepangwa kufanyika katika miji muhimu ya nchi hiyo ikiwemo ya Dodoma, Mwanza, Tanga, Kigoma na Zanzibar.
Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia kimetangaza kwamba kitaandaa mashindano ya Qur'ani katika majengo ya kitengo hicho mjini Dar es Salaam ambapo mashekhe mashuhuri wa Kishia na Kisuni wa Tanzania wamealikwa kushiriki. Mashindano kama hayo pia yamepangwa kufanyika katika madrasa za Thaqalain, Waliyu Asr (af) na Dar al- Huda mjini Dar es Salaam.
Maonyesho ya Qur'ani na kusoma juzuu moja ya Qur'ani kila siku katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo Waiarani wanoishi mjini humo wanatazamiwa kushiriki, ni miongoni mwa ratiba nyingine za kitengo hicho cha utamaduni. 1058088
captcha