Katika ujumbe wake Rais Kibaki amewataka Waislamu kuomba dua kwa ajili ya amani na umoja wa kitaifa nchini Kenya.
Kibaki amesema Mwezi wa Ramadhani ni kipindi muhimu katika kalenda ya Waislamu kote duniani kwani wanajisafisha kiroho na kuonyesha ukarimu.
Rais Kibaki pia amewataka Wakenya wote kuungana na Waislamu katika kutafakari kuhusu uhusiano wao na Mwenyezi Mungu na kuwasaidia watu wasiojiweza katika jamii. Rais wa Kenya amewatakia Waislamu kila la kheri katika mwezi huu wa Ibada.
Waislamu nchini Kenya wameanza mwezi mtukufu wa Ramadhani siku ya Jumamosi kufuatia tangazo la Kadhi Mkuu Sheikh Sharif Al Muhdhar.
Sheikh Muhdhar amewataka Waislamu wa Kenya wadumishe umoja katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Aidha amewataka Waislamu wenye uwezo kutoa misaada kwa wasiojiweza katika jamii
1058594