Katika ujumbe wake amesema: ‘ Sisi Waislamu tumebahatika kuwa na kitabu cha Qur'ani na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Pamoja na kuendesha ibada za Saumu, Sala na utoaji Sadaka katika mwezi huu, tutapata thawabu zaidi ikiwa tutazidisha kusoma na Qur'ani pamoja na Hadith za Mtume Muhammad, S.A.W. katika mwezi huu.’
Rais Shein ameashiria kuharibika maadili Zanzibar na kusema, ‘tukirejea kwenye Qur'ani na Hadith za Bwana Mtume S.A.W. tutajisaidia kupata suluhisho. Tukumbuke kuwa Quran Tukufu inanufaisha kila pahala na kila zama’.
Aidha Rais wa Zanzibar amewataka Wazanzibar wote waungane na amekumbusha mafundisho ya Qur’ani kuhusu umoja katika Surat Al – Imran, Aya 103 inayosema:
“Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu; vile mlivyokuwa nyinyi kwa nyinyi maadui, naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu”.
Rais Shein pia ametuma risala yake ya rambi rambi kufuatia ajali ya hivi karibuni ya meli Zanzibar iliyopelekea karibu watu 60 kuaga dunia. Zanzibar ni eneo lenye mamlaka ya ndani Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Karibu asilimu 99 ya watu wake wote ni Waislamu.
1059218