IQNA

Hafla ya kuhitimisha Qur'ani na usiku wa mashairi ya Kiislamu yafanyika mjini Istanbul

17:40 - July 23, 2012
Habari ID: 2375756
Hafla ya kuhitimisha Qur'ani Tukufu na usomaji wa mashairi ya Kiislamu ilifanyika siku ya Jumamosi katika Msikiti wa Zeinabiyya (as) katika mji wa Istanbul nchini Uturuki.
Shughuli hiyo na nyingine kama vile za utoaji hutuba za kubainisha fadhila na amali za mwezi wa Ramadhani, ratiba maalumu za wanawake na watoto na chakula cha futari zitatekelezwa msikiti hapo katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Imam wa msikiti huo Sheikh Hamit Turan amefafanua suala hilo na kuelezea matumaini yake kwamba mwezi huu mtukufu utawaletea Waislamu utulivu wa nyoyo, amani kwa mataifa yote na kuondoa dhulma na uonevu duniani.
Vilevile Ali Ozgunduz, mbunge wa chama cha Republican People's Party (CHP) alizungumza katika hafla hiyo na kusema kuwa mwezi wa Ramadhani ni fursa yenye thamani kubwa kwa ajili ya Waislamu kutekeleza ibada zao na kuongeza kuwa kutekelezwa kwa hafla kama hiyo ya kimaanawi msikitini kuna nafasi muhimu katika kuimarisha umaanawi wa waumini wanaosimamisha swala. 1060168
captcha