Akizungumza alipotemebela kibanda cha IQNA katika Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran, Seyyid Muhammad Husseini amepongeza IQNA kwa kuongeza idadi ya lugha zake hadi 40.
Huku akiwashukuru waandishi wa IQNA kwa juhudi zao, amewataka kuzidisha harakati zao kwa raghba kubwa zaidi ya huko nyuma.
Amesema ili kuwa na jamii bora, kuna haja ya kusambaza habari kuhusu harakati za Qur'ani.
Aidha ameyataja Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani kuwa tukio kubwa ambalo halina mfano wake duniani.
Maonyesho hayo ya mwezi moja yanatazamiwa kuendelea hadi tarehe 25 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
1059846