Akizungumza katika hafla hiyo, Muhammad Ridha Sulhju, mwanachama wa bodi ya wasimamizi wa Darul Qur'anil Karim amesema kwamba Wairani wana uzoefu wa miaka 50 wa kunufaika na mbinu za usomaji Qur'ani za Wamisri na kwamba kwa uchache Wairani wapatao 50 huwa wanasoma kwenye idhaa za taifa kwa mbinu hizo.
Amesema kwa baraka za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hivi sasa mafundisho ya usomaji Qur'ani, hifdhi na maarifa ya Qur'ani Tukufu yameenea katika pembe zote za nchi ambapo hii leo kuna mamia ya makari na mahafidh wa Qur'ani katika kila mji na kijiji nchini Iran.
Baada ya kutolewa hutoba za kuukaribisha ujumbe huo, ujumbe huo ulitemebelea sehemu na vitengo tofauti vya Darul Qur'anil Karim ambayo hujishughulisha na masuala mbalimali ya uchapishaji, usahihishaji, tathmini na usimamiaji wa masuala ya kitabu hicho kitakatifu.1060948