Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ISESCO, limepanga kupongeza na kumshukuru Hasna Khulali, mshindi wa kwanza wa mashindano ya Qur'ani Tukufu yaliyofanyika hivi karibuni nchini malaysia.
Shughuli hiyo itafanyika katika sherehe maalumu ambayo imepangwa kufanyika hapo kesho Jumatano katika mji wa Rabat.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Yaum Sabe' linalochapishwa nchini Misri, Bi Khulali alishinda mashindano hayo katika kitengo cha wanawake.
Katika sherehe hizo, Abdul Aziz bin Uthman at-Tuweijiri, mkuu wa ISESCO atamtunukia Bi Khulali medali na cheti maalumu cha shukrani cha shirika hilo kutokana na shughuli zake maalumu za Qur'ani. Isesco ina mchango muhimu katika kuhamasisha hifdhi, kiraa na maarifa ya Kiislamu katika shule za Qur'ani katika shule nyingi za nchi wanachama wa OIC.
Mashindano ya Qur'ani ya Malaysia ambayo yalifanyika katika makundi mawili ya wanaume na wanawake yalifanyika tarehe 6 hadi 13 Julai mjini Kuala Lumpur na kuwashirikisha makarii wa kike na wa kiume 60 kutoka nchi 42 za dunia.
Mashindano hayo ambayo yanahesabiwa kuwa ya zamani zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu yanasimamiwa na Taasisi ya Ustawi wa Kiislamu ya Malaysia. 1060325