IQNA

Mamia ya nakala za Qur'ani zatawanywa kwa mayatima wa Indonesia

15:42 - July 25, 2012
Habari ID: 2377486
Shirika la SinarMas ambalo ni moja ya mashirika ya uzalishaji vyakula na mazao ya kilimo mjini Jakarta nchini Indonesia limesambaza mamia ya nakala za Qur'ani Tukufu miongoni mwa mayatima wa mji huo kama zawadi za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Shirika hilo lilitoa nakala hizo hapo jana katika karamu maalumu ya iftari kwa ushirikiano wa Wizara ya Elimu na Utamaduni ya Indonesia. Suhendra Wiryadinata, Waziri wa Elimu na Utamaduni pamoja na Mkuu wa Uhusiano wa Umma wa shirika hilo walihudhuria karamu hiyo na kutoa hutuba kuhusiana na fadhila za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Katika mwezi huu mashirika mengi makubwa ya nchi hiyo huandaa futari na kutoa misaada kwa mayatima ili kunufaika na fadhila za mwezi huu. 1061903
captcha