Kwa mujibu wa tovuti ya akhbarak, Swalah Sultan amesema katika sherehe za ufunguzi wa chuo hicho kwamba muda wa kuhitimu katika chuo hicho utakuwa wa miaka minne. Ameongeza kuwa masomo yatakuwa yakianza mwanzoni mwa mwezi wa Septemba na kumalizika mwezi Mei.
Chuo hicho kitakuwa kikitoa mafunzo mbalimbali yanayohusiana na Qur'ani kama vile muujiza wa Qur'ani, elimu nafsi, elimu jamii, kuufahamu ulimwengu, sheria za Qur'ani na mbinu za Qur'ani kwa ajili ya kujirekebisha kimaadili.
Masharti ya kujiunga na chuo hicho ni pamoja na kujua vyema kiraa na sheria za tajwidi za Qur'ani Tukufu pamoja na kuwa na alama nzuri na za juu katika masomo ya chuo kikuu na kuhifadhi kwa uchache juzuu tatu za Qur'ani Tukufu.
Chuo hicho pia kitakuwa kikijishughulisha na masuala ya kutoa huduma za kijamii, kielimu na kiutafiti pamoja na vifurushi maalumu vya mwezi wa Ramadhani kwa wakazi wa mji huo wa Bani Suwayf. 1061459