IQNA

Rais aliyepinduliwa wa Tunisia aliufanyia hiana Uislamu

18:47 - August 15, 2012
Habari ID: 2393999
Rais Munsif Marzuqi wa Tunisia jana Jumanne aliwakosoa vikali watawala wa Saudi Arabia kwa kumpa hifadhi Zeinul Abedin bin Ali dikteta wa zamani wa Tunisia ambaye amesema aliufanyia hiana kubwa Uislamu katika kipindi cha utawala wake.
Rais Marzuqi amewataka viongozi wa Riyadh wamkabidhi haraka dikteta huyo kwa serikali ya Tunisia, dikteta ambaye amesema aliufanyia hiana kubwa Uislamu, kuvunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qura'ni na vilevile kupora mali za raia wa nchi hiyo.
Ameshangazwa na ukweli kuwa Saudi Arabia imempa hifadhi mhalifu huyo ambaye amefanyia hiana Uislamu na kuivunjia heshima mara kadhaa Qur'ani Tukufu wakati wa utawala wake wa kiimla nchini Tunisia.
Rais wa Tunisia amesema suala la kurejeshwa Bin Ali nchini Tunisia ili ahukumiwe na mahakama za nchi hiyo ni jambo muhimu litakaloainisha mustakbali wa uhusianao wa nch mbili hizo.
Rais Marzuqi ambaye yuko mjini Makka Saudi Arabia kwa lengo la kuhudhuria kikao cha viongozi wa nchi wanachama wa OIC amesisitiza kwamba mwenendo wa demokrasia nchini humo unaendelea na kwamba uchaguzi mkuu ujao utafanyika mapema mwakani. 1079271
captcha