Ayatullah Muhammad Imami Kashani amesema hayo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya kimaanawi na kisiasa ya Sala ya Ijumaa na kusisitiza kwamba, masuala yaliyojadiliwa katika mkutano huu wa NAM yalikuwa muhimu mno. Ayatullah Kashani amesema, Mkutano wa Wakuu wa NAM hapa Tehran ni tukio muhimu katika jitihada za kusukuma mbele gurudumu la malengo ya jumuiya hiyo. Amesema, uwenyekiti wa Iran wa miaka mitatu wa jumuiya hii kubwa zaidi baada ya Umoja wa Mataifa unaweza kusaidia kuharakisha kufikiwa malengo ya NAM katika uga wa kimataifa. Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameitaka NAM ifanye jitihada za kuhitimisha uvamizi wa utawala wa Kizayuni wa Israel huko Palestina na kuleta mabadiliko katika muundo wa Umoja wa Mataifa.
1088405