Mjini London huko Uingereza Waislamu walifanya maandamano makubwa jana wakilaani filamu hiyo na kutoa wito wa kupasishwa sheria inayopiga marufuku kuvunjiwa heshima matukufu yaa Uislamu.
Miji mbalimbali ya Iran ukiwemo mji wa Qum imeshuhudia mikusanyiko na maandamano ya kulaani filamu hiyo; ambapo waandamanaji walijitokeza katika bararaba za miji hiyo na kupaza sauti wakilaani filamu hiyo. "Mauti kwa Marekani", "Mauti kwa Israel" na "Labbaika Yaa Muhammad" ni baadhi ya nara zilizopigwa na waandamanaji katika mudhahara huo ambapo walikuwa wamebeba mabango na maberamu yaliyokuwa na maandishi ya yaliyokuwa na jumbe mbalimbali.
Mji wa Karachi nchini Pakistan, nao umeshuhudia maandamano makubwa ya Waislamu ya kulaani filamu hiyo ya Kimarekani inayomtusi na kumvunjia heshima Mtume wa Uislamu.
Wakati huo huo, habari kutoka London Uingereza zinasema kuwa, Waislamu wa mji huo wameandamana na kulaani filamu hiyo huku wakitoa wito wa kupasishwa sheria za kupiga marufuku kuvunjia heshima Uislamu na matukufu yake.