Almanar imeonyesha video ya safari hiyo ambayo imefichua udhaifu mkubwa wa jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel. Kwa mujibu wa video hiyo, ndege isiyo na rubani ya Hizbullah ilikaribia kabisa kiwanda cha nyuklia cha Demona cha utawala wa kizayuni bila ya kugunduliwa na rada za kisasa za Tel Aviv. Baadaye ndege hiyo isiyo na rubani ilionekana na kuangushwa na jeshi la wazayuni. Akizungumzia tukio hilo, Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah amesema wanamuqawama wako imara zaidi hivi sasa ikilinganishwa na huko nyuma na kwamba utawala wa kizayuni ni dhaifu zaidi hivi sasa ikilinganishwa pia na huko nyuma. Tukio hilo limemtia aibu Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ambaye amelazimika kuitisha uchaguzi wa mapema miezi 9 kabla ya tarehe iliyokuwa imepangwa.
1118672