Kitendo hicho kiovu kinafuatia kushadidi kwa wimbi la kuchafuliwa jina la dini hiyo ya Mwenyezi Mungu barani Ulaya. Wimbi hilo linatokana na woga wa makundi hayo wa kasi ya kuenea Uislamu na mafundisho yake katika nchi za bara hilo.
Habari zinasema kuwa Muislamu mmoja aliyekuwa amekwenda kwenye msikiti wa eneo la Tournai alfajiri ya tarehe 4 Disemba alikuta nakala ya Qur'ani iliyochomwa nusu ikiwa imebandikwa katika mlango wa msikiti huo.
Ijumaa iliyopita pia barua moja ambayo haikuwa na anwani ya mtumaji wake ilitumwa kwenye msikiti huo ikidai kuwa Uislamu inaelekea kuangamizwa.
Hii si mara ya kwanza kufanyika kitendo kama hicho katika eneo hilo la Ubelgiji. Mwezi uliopita pia barua kadhaa zinazohujumu Uislamu zilisambazwa katika masanduku ya posta ya wakazi wa mji huo. 1148678