IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yaanza leo Libya

19:48 - December 08, 2012
Habari ID: 2460078
Mashindano ya 8 ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Libya yameanza leo mjini Tripoli.
Mashindano hayo yanasimamiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Libya katika Hoteli ya Corinthia.
Muhammad Rabo ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya mshindano hayo ya Qur'ani amesema kuwa nchi 120 zilialikwa kushiriki katika mashindano hayo na kwamba baadhi ya nchi hizo zinashiriki.
Kamati ya majaji wa mshindano hayo inaongozwa na Sheikh Rushdi al Suwaid kutoka Syria akishirikiana na majaji wengine kutoka Libya, Tunisia, Uturuki na Burkina Faso.
Abdur Rahman Mujli kutoka mji wa Benghazi ambaye mwaka 2010 alishika nafasi ya pili katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Algeria ndiye anayewakilisha Libya katika mashindano ya sasa ya Tripoli.
Mshindi wa kwanza wa mashindano hayo atapewa zawadi ya dinari laki moja za Libya, wa pili elfu 80, wa tatu elfu 60, wanne elfu 40 na wa tano elfu 20.
Washiriki katika mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani wanapaswa kuwa na umri usiozidi miaka 25, wawe wamehifadhi Qur'ani nzima na wawe raia wa nchi wanazowakilisha.
Katika mashindano hayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inawakilishwa na Hussein Kuhkheil kutoka mkoa wa Alborz. 1149565
captcha