Katika hifdhi ya Qur'ani nzima pamoja na kiraa na tajwidi, Tanwir Hussein Muhammad Ilyas kutoka Bangladesh ameshika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Abdullah bin Salah Hamdan al Saidi kutoka Saudia. Nafasi ya tatu katika kitengo hiki imeshikwa na Abdur Rahman Ihab Awadh kutoka Yemen.
Katika hifdhi ya juzuu 20 za Qur'ani, kiraa na tajwidi, Muhammad Ihsanuddin kutoka Bangladesh pia ameshika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Umar Abdul Karim Khalil kutoka Jordan na Abdur Rahman Khalid Latif wa Saudia ambaye ameshika nafasi ya tatu.
Mbangladesh mwingine Muhammad Saad ameshika nafasi ya kwanza katika hifdhi ya juzuu 10 akifuatiwa na Muhammad Bishara Abkar kutoka Cameroon na Khalid Abdulsalaam Muhammad wa Morocco.
Katika mashindano ya hifdhi, kiraa na tajwidi ya juzuu tano za Qur'ani, karii Muhammad Razqan kutoka Sri Lanka ameshika nafasi ya kwanza na nafasi ya pili imechukuliwa na Haris Yusuf Ali kutoka visiwa vya Réunion. Nafasi ya tatu imechukuliwa na Muhammad Maamaa kutoka Thailand.
Na katika hifdhi ya Qur'ani nzima, tajwidi na tafsiri, Msaudia Abdulmajid bin Muhammad Falata ameshika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Muhammad Irshad Lakhdar kutoka Algeria na Mazin Salah Ali Mahjub kutoka Sudan.
Viongozi wa Saudi Arabia hawakuwaalika makarii wa Qur'ani kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mwaka wa pili mfululizo.
Viongozi wa Jumuiya ya Wakfu ya Iran wanasema kutoalikwa wasomaji Qur'ani wa Iran kunatokana na ama masuala ya kisiasa au uwezo mkubwa wa makarii wa Jamhuri ya Kiislamu, kwani maafisa wa Saudia hawataki kuona Wairani wakishinda mashindano hayo. 1150855