IQNA

Sudan kutangaza ujumbe wa Qur’ani Afrika na duniani

20:29 - December 22, 2012
Habari ID: 2468193
Makamu wa Rais wa Sudan ametangaza kuwa nchi hiyo imeazimia kuzidisha uchapishaji wa nakala za Qur’ani Tukufu na kueneza mafundisho ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu barani Afrika na dunia kote.
Alhaj Adam Yusuf ameyasema hayo katika mkutano wake na maafisa wa Nyumba ya Qur’ani Afrika mjini Khartoum na kuzitaka jumuiya na taasisi mbalimbali za Sudan kusaidia uchapishaji wa nakala za Qur’ani Tukufu na kutangaza ujumbe wa kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Vilevile Makamu wa Rais wa Sudan ametaka kuimarishwa suna ya kutoa wakfu Qur’ani Tukufu na kusisitiza kuwa juhudi za kueneza mafundisho ya Qur’ani zinapaswa kudumishwa.
Alhaj Adam amewapongeza viongozi wa Nyumba ya Qur’ani Afrika kwa kusaidia uchapishaji wa nakala za Qur’ani na kuzigawa kwa wasomaji wa kitabu hicho.
Sudan imekuwa mstari wa mbele katika suala la harakati za Qur’ani Tukufu na maeneo mbalimbali ya nchi hiyo yana madrasa na vituo cha kusoma na kuhifadhi Qur’ani. Nchi hiyo pia inasifika kwa kuwa na idadi kubwa ya mahafidhi wa Qur’ani Tukufu. 1157998
captcha