Athari hizo zilizogunduliwa katika paa la msikiti wa Jamia wa Sanaa zinarejea katika karne ya kwanza Hijria na zinajumuisha nakala moja ya Qur'ani ambayo sehemu yake kubwa haijaharibika.
Naibu Waziri wa Utamaduni wa Yemen A'mir al Ahmadi amesema kuwa miaka 40 iliyopita nakala za kale za Qur'ani pia zilipatikana katika msikiti huo wakati wa kukarabatiwa paa lake.
Amesema kuwa athari hizo za kale zilizopatikana katika msikiti mkuu wa Sanaa ni kielelezo kuwa Yemen ni jumba kubwa la makumbusho mbele ya wataalamu wa turathi za kale na kwamba bado hawajaweza kupata athari nyingi za kale za Kiislamu zilizoko nchini humo.
Msikiti wa Jamia wa Sanaa ndio mkongwe na wa kale zaidi nchini Yemen na inasemekana kuwa ulijengwa katika zama za Mtume Muhammad (saw).
Vyanzo vya historia vinasema kuwa, wakati Mtume (saw) alipomteuwa Wabar bin Yahnas al Ansari kuwa gavana wake huko Sanaa alimuamuru kujenga msikiti huo. 1166299