IQNA

Qur'ani, kitabu kinachouzwa kwa wingi zaidi India

10:30 - January 10, 2013
Habari ID: 2478396
Qur'ani na vitabu vya fasihi ya Kiislamu ndivyo vinavyouzwa kwa wingi zaidi katika tamasha ya vitabu nchini India ambayo inafanyika katika mji wa Vijaywada katika jimbo la Andhra Pradesh.
Tovuti ya The Hindu imeripoti kuwa kusoma na kuelewa Qur'ani na vitabu vya fasihi vya Kiislamu ilikuwa kazi ngumu kwa wananchi wa India kutokana na vitabu hivyo kuandikwa kwa lugha za Kiarabu, Kifarsi na Urdu.
Hata hivyo tamasha ya vitabu ya Vijaywada imepunguza kwa kiasi kikubwa tatizo hilo kwa kuuza nakala za Qur'ani na vitabu vya fasihi ya Kiislamu kwa lugha za Kiingereza na Telgu.
Wasimamizi wa tamasha hiyo wanasema kuwa tarjumi ya Qur'ani Tukufu kwa lugha za Kiingereza na Telgu zinauzwa kwa wingi zaidi ya vitabu vingine katika tamasha hiyo.
Baada ya Qur'ani, vitabu vingine vinavyouzwa zaidi ni vile vinavyozungumzia maisha ya Mtume Muhammad (saw), swala na Mwenyezi Mungu SW, wanawake katika Uislamu na Qur'ani ya Sayansi.
Tamasha ya vitabu ya Vijaywada hufanyika kila mwaka kuanzia Januari Mosi hadi tarehe 11. 1169174

captcha