IQNA

Shahat, mgeni wa fahari wa mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Iran

10:30 - January 10, 2013
Habari ID: 2478397
Ustadh Mahmoud Shahat, karii na msomaji mashuhuri wa Qur'ani wa Misri atakuwa mgeni wa heshima katika mashindano ya 35 ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu nchini Iran.
Mashindano hayo yataanza tarehe 27 Januari katika mji wa Sari, makao makuu ya mkoa wa Mazandaran huko kaskazini mwa Iran sambamba na maadhimisho ya sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Ustadh Shahat atasoma Qur'ani katika mashindano hayo yatakayowashirikisha maqari na mahafidhi wa Qur'ani 200 wa kike na makari na mahafidhi 200 wa kiume.
Sheikh Mahmoud ni mwana wa Ustadh Shahat Anwar na alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani nzima akiwa na umri wa miaka 12. Mwaka huo huo Mahmoud Shahat alishinda nafasi ya kwanza ya mashinano ya kimataifa ya Qur'ani ya "Lailatul Qadr" nchini Misri na anasema mafanikio hayo ni matunda ya jitihada kubwa za marehemu baba yake. 1169139


captcha