Mashindano hayo ya siku tatu yalimalizika Alkhamisi 24 Januari ambapo kulikuwa na vitengo vinne vya qiraa ya Qur’ani Tukufu na hifadhi ya juzuu 5, juzuu 15 na Qur’ani kamili.
Mashindano hayo yaliandaliwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Katika kitengo cha qiraa ya Qur’ani Tukufu, Mehdi Saeedi ameshika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Alaeddin bin Hajj kutoka Brunei, Mohamoud Noor-Mohammad kutoka Malaysia, Tariq Elham kutoka Palestina na Muhammad Yunis Alawi kutoka Afghanistan kwa taratibu.
Katika kitengo cha kuhifadhi Qur’ani nzima, Hassan Rajabi ameibuka mshindi akifuatiwa na Balal Ahmed kutoka Pakistan, Othman Ahmed Mahmoud wa Sudan, Muhammad Saleh Baldi kutoka Guinea Conakry na Abdullah Muhammad Abuasil kutoka Jordan.
Katika kitengo cha hifdhi ya juzuu tano vilevile mwakilishi wa Iran, Muhammad Sharifi amshika nafasi ya kwanza na kufuatiwa na Khalil Al-Saeedi wa Oman, Muhammad Noorasalam wa Bangladesh, Muhammad Shahed kutoka Pakistan, na Darid Al-Daridi wa Jordan.
Katika kitengo cha kuhifadhi juzuu 15 nafasi ya kwanza imechukuliwa na Falah Fazalan wa Sudan. Washindi wengine katika kitengo hicho kwa taratibu walikuwa ni Bassam Mahmoud wa Jordan, Waqar Ahmed kutoka Pakistan, Sayyid Hamid Rezaee wa Iran na Rahimullah Rahmani kutoka Afghanistan. Washindi katika kila kitengo walipata zawadi ya pesa taslimu pamoja na cheti cha heshima.
1177239