Nakala hizo za kale za Qur'ani zimegunduliwa katika msikiti wa wilaya ya Qaunia na inakadiriwa kuwa zina umri wa zaidi ya miaka 200.
Nakala hizo za Qur'ani ambazo zimeandikwa miaka 200 hadi 250 iliyopita zimegunduliwa wakati wa kufanya usafi kwenye paa la msikiti na maktaba yenye turathi za maandishi ya hati za mkono.
Mkuu wa maktaba ya Qaunia amesema kuwa nakala hizo 32 za Qur'ani zitakarabatiwa katika kipindi cha mwaka mmoja na kuoneshwa wka watu wote.
amesema hii si mara ya kwanza kugundyliwa nakala za kale za Qur'ani katika eneo hilo.1180206