Katika maandamano hayo ambayo yalitayarishwa na harakati ya Hamas, Waislamu wa Palestina wamelaani vikali kitendo kiovu cha askari wa Israel cha kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu ndani ya Msikiti wa al Aqsa.
Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina Ismail Hania ambaye alihutubia Swala ya Ijumaa ya jana aliwahimiza wananchi wa Palestina kushikamana na kuwa na umoja mbele ya hila na njama za Wazayuni wa Israel.
Baada ya Swala hiyo ya Ijumaa Wapalestina walielekea kwenye jengo la Bunge kutangaza hasira yao kubwa dhidi ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.
Jumapili iliyopita afisa mmoja wa polisi ya Israel alivamia kikao cha kiraa ya Qur'ani cha wanawake ndani ya Msikiti wa Al Aqsa na kukivunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani kwa kukipiga teke. 1201059