IQNA

Wawakilishi wa nchi 50 kushiriki mashindano ya kimataifa ya Qur’ani, Kuwait

18:54 - March 13, 2013
Habari ID: 2511104
Duru ya nne ya mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu nchini Kuwait itaanza tarehe 3 Aprili ikiwashirikisha wawakilishi wa nchi 50.
Shirika rasmi la habari la Kuwait KUNA limemnukuu Naibu Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Kuwait Adil al Fallah akisema kuwa, mashindano ya hifdhi, tajwidi na kiraa ya Qur’ani Tukufu Tuzo ya Kuwait yatafanyika katika fremu ya shughuli zinazohusu Qur’ani za wizara hiyo. Amesema mashindano hayo yataanza tarehe 3 Aprili yakisimamiwa na Amir wa Kuwait, Sabah Ahmad Jabir al Sabah na kumalizika tarehe 10 Aprili.
Naibu Waziri wa Wakfu wa Kuwait amesema kuwa nchi 63 zilialikwa kushiriki katika mashindano hayo na kwamba ni nchi 50 tu ndizo zilizotangaza kwamba zitashiriki.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itawakilishwa na karii wa kimataifa wa Qur’ani Tukufu Sayyid Mustafa Hussain na Hussein Mahdizadah katika mashindano hayo ya Kuwait. 1203714
captcha