IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur’ani yaanza Sulaimaniya

18:54 - March 13, 2013
Habari ID: 2511105
Duru ya kwanza ya mashindano ya kimataifa ya hifdhi na kiraa ya Qur’ani imeendelea huko Sulaimaniya katika eneo la Kurdistan huko kaskazini mwa Iraq.
Tovuti ya Kurd Press imeripoti kuwa, mashindano hayo ya kimataifa ya Qur’ani yanawashirikisha makarii kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Iran, Algeria, Misri na Bangladesh.
Mashindano hayo yanasimamiwa na serikali na eneo hilo kwa kushirikiana na Shirika la Wakfu la mkoa huo.
Lengo la mashindano hayo ambayo yatakuwa yakifanyika mara kwa mara nchini Iraq ni kustawisha zaidi ustaarabu wa kitabu kitukufu cha Qur’ani na kuwaarifisha Waislamu wa Kikurdi. Mashindano hayo yaliyofunguliwa Jumatatu iliyopita yanamalizika leo Jumatano. 1203766
captcha