IQNA

Wanawake wa Kipalestina walaani kuvunjiwa heshima Qur'ani

21:44 - March 16, 2013
Habari ID: 2511985
Wanawake wa Palestina waliandamana jana ndani ya Msikiti wa al Aqsa wakilaani kitendo cha askari wa utawala ghasibu wa Israel cha kuvunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani.
Katika maandamano hayo wanawake hao waliweka nakala za Qur'ani Tukufu juu ya vichwa vyao na kulaani vikali kitendo cha afisa mmoja wa polisi ya Israel cha kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu ndani ya Msikiti wa al Aqsa.
Waandamanaji hao pia wamewataka wanawake, vijana, wanaume na maulamaa wa Palestina kuulinda Msikiti wa al Aqsa mbele ya hujuma na mashambulizi ya Mayahudi wenye misimamo mikali.
Tarehe 3 Machi afisa mmoja wa polisi ya Israel aliingia ndani ya Msikiti wa al Aqsa na kuvamia kikao cha kiraa ya Qur'ani cha wanawake na kuzipiga teke nakala za Qur'ani Tukufu. 1204816

captcha