Mkurugenzi wa Baitul Qur'ani ya Kuwait, Nasir al Dabbus ambaye ndiye mwenyekiti wa mashindano hayo amesema kuwa awamu ya kwanza ya mashindano hayo imemalizika na kwamba tume ya mashindano hayo itaanza kuwasiliana na washiriki wa awamu ya mwisho.
Nasir al Dabbus amesema kuwa, mashindano hayo yanafanyika katika vitengo vinne vya watoto wadogo, mabarobaro, vijana na watu wazima. Ameongeza kuwa mwaka huu kitengo cha watu wazima kinawashirikisha raia wa Kuwait na wa nchi za nje wanaoishi nchini humo.
Amesema kuwa awamu ya kwanza ya mashindano hayo ya Qur'ani lifanyika katika mikoa sita ya Kuwait na kwamba kamati 24 zilizimamia mashindano hayo.
Amesema raia wa nchi 46 wanaoishi Kuwait wameshiriki katika awamu ya kwanza na kwamba idadi ya washiriki imeongezeka ikilinganishwa na miaka iliyopita. 1205972