Gazeti la al Dustur linalochapishwa Jordan limeandika kuwa, Harakati ya Hirakul Aimma imetangaza kuwa: Kinachoumiza moyo zaidi ni kwamba kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu kimefanyika katika moja ya vituo vya elimu na maarifa tena kilichopewa jina la Aalul Bait wa Mtume Muhammad (saw).
Taarifa hiyo imesema: Kitendo hicho kinaonesha kuwa mporomoko wa maadili umefikia kiwango kikubwa sana cha kuvunjiwa heshima sheria za kidini na thamani za kibinadamu.
Harakati ya Hirakul Aimma imewataka wananchi wote kukabiliana na vitendo vyote vya utovu wa maadili na kutetea haki na uadilifu ambavyo vimetiliwa mkazo katika Qur'ani Tukufu.
Siku chache zilizopita kundi moja la wanafunzi wa Kitengo cha Uchumi cha Chuo Kikuu cha Aalul Bait nchini Jordan lilikamatwa na askari wanaolinda chuo hicho kwa kosa la kuvunjia heshima Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Wanafunzi hao ni wafuasi wa kundi la watu wanaoabudu shetani. 1205873