Akizungumza Ijumaa alasiri hapa mjini Tehran, Hujjatul Islam wal Muslimin Mohammadi Golpaygani ametoa hotuba kuhusu umuhimu wa kutekeleza mafundisho ya Qur’ani Tukufu na Jihad katika njia ya Allah SWT.
Katika hotuba yake ameashiria aya ya 24 ya Surat al Anfaal katika Qur’ani Tukufu inayosema: "Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” Amesema Allamah Majlisi na Fakhr Razi katika kuifasiri aya hii wameitaja kuwa inayobainisha Imani na Uislamu.
Sheikh Golpaygani amesema iwapo katika ulimwengu wa Kiislamu Jihadi katika njia ya Allah itahuishwa kwa maana yake halisi basi hali ya Waislamu itabadilika na kuboreka.
Ameongeza kuwa Qur’ani Tukufu imeharamisha ribaa lakini kutokana na kuenea riba katika ulimwengu wa leo hali imekuwa mbaya sana na aghalabu ya watu wanakumbwa na njaa huku utajiri ukiwa katika mikono ya wachache. Amesema wakati Imamu wa zama, Imam Mahdi (Allah aharakishe kudhihiri kwake) atakaporejea, atairekebisha jamii kwa kutumia Qur’ani Tukufu kiasi kwamba hakutakuwa na masikini wa kupokea Zaka duniani.
Mashindano ya 30 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanahudhuriwa na washirki 111 kutoka nchi 75 za mabara matano ya dunia. Mashindano hayo yameanza leo Ijumaa tarehe 20 Rajab na yatamalizika Ijumaa tarehe 27 Rajab kwa mnasaba wa Siku ya Mabaath.
1236491