Akizugumza Jumanne katika kikao chake na mubalighina wa mwezi wa Muharram, Sayyid Hassan Nasrallah amesema kile kilichojiri Mina ni ushahidi wa wazi wa muamala usio wa kibinadamu wa watawala wa Saudia kwani walifanya makusudi kutowasaidia mahujaji waliokuwa katika hali ngumu sana.
Sayyid Nasrallah ameongeza kuwa utawala wa Saudia unalenga kuvuruga kambi ya mapambano inayojumuisha Iran, Russia na Venezuela kwa kushusha bei ya mafuta ghafi duniani. Kiongozi wa Hizbullah amesema, ‘Israel inajaribu kufelisha mapatano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 lakini imeshindwa kwani mkataba huo umefikiwa kwa busara ya Iran na kwamba hivi karibuni Iran itapata fursa nyingi kufuatia mapatano hayo. Sayyid Nasrallah amesisistiza umoja wa Kiislamu katika hali ya sasa duniani huku akisisitiza kuwa Ahul Sunna si wakufurishaji na wala wao si Mawahabi ambao ni sehemu ndogo sana ya Waislamu zaidi ya bilioni moja duniani. Katika sehemu nyengine ya hotuba yake, Sayyid Nasrallah amesema makundi ya kigaidi ya Daesh yaani ISIS, al Qaeda na Jabhatu Nusrsa yanahudumia Wazayuni ambao wanataka kuona serikali ya Syria inaanguka.../mh