Marasimu hizo hufanyika kukumbuka kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS na wafuasi wake watiifu 72 katika jangwa la Karbala zaidi ya miaka 1,300 iliyopita.
Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo ya Waqfu nchini Misri imesema kuwa, itachukua hatua zote za kisheria kwa mtu yeyote atakayevunja amri hiyo katika msikiti huo. Kufuatia hali hiyo, Dakta Ahmed Rasim al-Nafis, kiongozi mkuu wa Waislamu wa Kishia nchini Misri sanjari na kukosoa amri hiyo, amesema kuwa hatua ya kufunga msikiti huo wa Imamul-Hussein kwa lengo la kuwazuia Waislamu wa Kishia kuhuisha kumbukumbu za tukio la mauaji ya Ashura, dhidi ya mjukuu wa Mtume wa Waislamu, ni kwenda kinyume na sheria ya uhuru wa kuabudu kama vile ambavyo pia ni kutii fikra za Kiwahabi zilizojikita katika Chuo cha al-Azhar cha nchi hiyo. Aidha Dakta Rasim al-Nafis ameongeza kuwa, sheria hiyo mbali na kwamba haina mantiki yoyote, pia haina mashiko, kwani hata kabla ya hapo Waislamu wa Kishia nchini humo hawakuwa na nia yoyote ya kufanya marasimu hayo katika eneo hilo. Amesema kuwa, kila mwaka serikali ya Misri imekuwa ikizuia kufanyika marasimu ya kumbukumbu za tukio la Ashura, suala ambalo linathibitisha ni kwa kiasi gani Waislamu wa Kishia nchini humo wanavyokabiliwa na hatari kubwa kutoka kila upande ikiwemo serikali ya Cairo. Amekosoa nafasi ya chuo kikuu cha al-Azhar nchini Misri kama taasisi kuu inayosimamia masuala ya Waislamu wa madhehebu zote kwa kushindwa kukemea suala hilo na kuongeza kuwa, badala ya viongozi wa chuo hicho kutetea kila upande, wamebakia tu wakipendelea maslahi ya upande mmoja na hivyo kukiuka misingi yake mikuu ya kuwaunganisha pamoja Waislamu, suala ambalo linathibitisha kujikita fikra za Kiwahabi katika taasisi hiyo kubwa ya kidini nchini Misri na duniani kwa ujumla..../mh