IQNA – Mamilioni ya waombolezaji mjini Karbala wameshiriki adhuhuri ya Ijumaa ya Ashura katika msafara mkubwa na wa kihistoria wa Rakdhat Tuwairij.
Habari ID: 3482410 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/27
IQNA – Ukiendelea na mnyororo wake wa kimfumo wa kuzuia uhuru wa maoni na kukandamiza wataalamu na watendaji wa kiraia, ufalme wa kiimla wa Bahrain umemkamata mtafifi mwelekeo wa Shia.
Habari ID: 3482408 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/27
IQNA – Hafla ya kisomo cha Qur’ani Tukufu imefanyika siku ya Ashura katika mji mtukufu wa Karbala.
Habari ID: 3482407 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/27
IQNA-Waislamu wa mji wa Witu katika Kaunti ya Lamu, pwani ya Kenya wameshiriki katika maombolezo ya siku ya Ashura, ambayo ni kumbukumbu ya kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (SAW), Imam Hussein bin Ali (AS), watu wa nyumba yake na wafuasi wake watiifu katika uwanda wa Karbala, Iraq mwaka 61 Hijria Qamaria. Maadhimisho hayo yameandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Umul Banin mjini humo. Hizi hapa chini klipu za maombolezo hayo.
Habari ID: 3482406 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/26
IQNA – Haram takatifu ya Imam Hussein (AS) katika mji wa Karbala nchini Iraq ilijaa mazuwaru usiku wa kuamkia Ashura, ambao uliangukia usiku wa Alhamisi katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Habari ID: 3482405 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/26
IQNA – Hafla ya maombolezo ya Ashura iliandaliwa siku ya Ijumaa kwenye kaburi la shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa harakati ya mapambano ya Hizbullah ya Lebanon.
Habari ID: 3482403 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/26
IQNA – Kwa mnasaba wa kuwasili kwa siku za Tasua na Ashura, yaani tarehe ya tisa na ya kumi ya mwezi wa Muharram, Jumuiya ya Qur'ani nchini Iran iliendesha ibada ya jadi ya Khatma ya Qur’ani, yaani usomaji wa Qur’ani Tukufu kuanzia mwanzo hadi mwisho wake.
Habari ID: 3482402 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/26
IQNA – Mwamko wa Imam Hussein (AS) haukuwa uasi wa kimageuzi uliotokea na kuishia katika kurasa za historia; bali ulikuwa ni mkondo wa kifikra wenye malengo matukufu na maadili ya kimalakuti yanayovuka mipaka ya zama.
Habari ID: 3482401 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/25
IQNA-Wairani katika mji mkuu Tehran, majiji, miji na vijiji vyote nchini usiku wa kuamkia leo walikusanyika misikitini na katika vituo vya kidini na barabarani katika marasimu ya kuadhimisha Tasu'a, siku ya tisa ya mwezi Muharram, kuelekea kwenye Siku ya Ashura ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW).
Habari ID: 3482397 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/24
IQNA – Tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Muharram wiki iliyopita, Waislamu wa madhehebu ya Shia wameandaa majlisi na shughuli za maombolezo kukumbuka kuuawa shahidi kwa Imam Hussein (AS) katika miji na majiji 400 nchini Niger na Nigeria.
Habari ID: 3482395 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/23
IQNA – Katika jitihada za kuimarisha usalama na kuhakikisha utulivu wakati wa siku tukufu za Tasua na Ashura katika mji mtakatifu wa Karbala, nchini Iraq, jumla ya kamera 2,000 za kisasa (smart cameras) zimewekwa kama sehemu ya mpango maalum wa kiusalama.
Habari ID: 3482392 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/23
IQNA – Mtafiti kutoka Lebanon ametoa uchambuzi wa kihistoria akichunguza jinsi mila za maombolezo kwa Imam Hussein (AS) na mashahidi wa Karbala zilivyobadilika katika karne tano za kwanza za kalenda ya Hijiria, akibainisha hatua tatu tofauti kuanzia huzuni ya binafsi hadi ibada ya hadhara.
Habari ID: 3482383 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/20
IQNA – Waislamu wa madhehebu ya Shia katika eneo la Qatif nchini Saudi Arabia wanaendelea kufanya majlisi na ibada za Muharram licha ya vizuizi vinavyoripotiwa kuwekwa na mamlaka.
Habari ID: 3482376 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/19
IQNA – Maombolezo ya Muharram si vitendo vya huzuni tu; bali kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia kote duniani, ni uhai wa imani iliyodumu kwa karne kumi na nne, amesema mwanazuoni mmoja wa Kiislamu.
Habari ID: 3482370 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/17
IQNA – Huku mwezi wa Muharram katika kalenda ya Hijria ukiwa umeingia, vikosi vya jeshi la Iraq vimeongeza kiwango cha utayari na doria ili kuhakikisha usalama wa misafara na mijumuiko maombolezo.
Habari ID: 3482366 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/16
IQNA – Katika kuukaribisha mwezi wa Muharram wa kalenda ya Hijria, Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) mjini Karbala, Iraq, imetangaza tarehe ya hafla ya kubadilisha bendera ya kuba la haram hiyo.
Habari ID: 3482364 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/15
IQNA – Kuta na viwanja vya makaburi au haram tukufu za Imam Hussein (AS) na Hadhrat Abbas (AS) katika mji wa Karbala, Iraq, vimepambwa kwa bendera nyeusi na alama za maombolezo huku mwezi wa Muharram wa kalenda ya Hijria ukikaribia.
Habari ID: 3482356 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/13
IQNA – Wakati mwezi wa Muharram unavyokaribia, vibali zaidi ya 700 vimetolewa kwa ajili ya kuanzisha maukibu mjini Karbala, kwa lengo la kuwahudumia waombolezaji wa Muharram katika mji huo mtukufu.
Habari ID: 3482348 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/10
IQNA-Maonyesho ya sanaa za Qur’ani na kidini yenye kichwa “Sanaa ya Mapenzi, Imani na Ashura” yalifanyika katika Chuo Kikuu cha Kashmir yakiratibiwa na Taasisi ya Utafiti wa Qur’ani ya Tebyan. Zaidi ya kazi mia moja za uchoraji, kaligrafia, picha na sanaa za kidigitali ziliwasilisha mada za Qur’an, Karbala na kujitolea.
Habari ID: 3481118 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/22
IQNA – Maonesho ya kaligrafia ya maandishi ya Kiarabu ya siku tatu yaliyopewa jina "Katika Njia ya Ashura" yamefunguliwa katika eneo tukufu la Bayn al-Haramayn—kati ya makaburi ya Imam Hussein (AS) na Hadhrat Abbas (AS) huko Karbala, Iraq.
Habari ID: 3480948 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/15