IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Sharm el-Sheikh Misri

13:31 - November 25, 2015
Habari ID: 3457049
Awamu ya 23 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Misri yatafanyika hivi karibuni katika mji wa Sharm el Sheikh mkoa wa Sinai.

Kwa mujibu wa gazeti la Al-Youm Al Sabi', Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu Misri imesema  mashidano hayo ya Qu'rani yanafanyika katika mji huo wa kitalii kwa lengo la kuimarisha utalii wa kidini katika eneo hilo.
Ingawa kumeripotiwa hujuma kadhaa za kigaidi katika Sinai, serikali ya Misri inasisitiza kuwa eneo hilo la kitalii bado ni salama.

Mashindano hayo ya Qur'ani yatafanyika katika kategoria kadhaa ikiwa ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani kikamilifu kwa kizingatia misingi ya tilawa. 
Washiriki katika mashindano hayo wanapaswa kuwa chini ya umri wa miaka 25 na hawapaswi kuwa wamewahi kushika nafasi ya kwanza katika mashindano yaliyopita ya Qur'ani.
Aidha kutakuwa na kategoria za kuhifadhi Qur'ani kikamilifu kwa washiriki walio chini ya umri wa miaka 12. Halikadhalika kutakuwa na kategoria ya kuhifadhi Juzuu tatu kwa walemavu.

3456547

captcha