Majid Pireh, afisa mwandamizi wa Shirika la Hisa la Iran (SEOI) amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa mkutano huo umepangwa kufanyika kuanzia Mei 2-4.
Amesema SEOI imeandaa mkutano huo kwa ushirikiano na Banki ya Maendeleo ya Kiislamu IDB.
Amebaini kuwa mkutano huo umeitishwa kwa lengo la kusahilisha maingiliano baina ya masoko ya kifedha yanayofuata mfumo wa Kiislamu duniani. Aidha amesema lengo jingine la kikao hicho ni kuarifisha mafanikio na ustawi wa sekta ya kifedha katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Majid Pireh amesema mkutano huo wa Tehran pia utajadili kwa kina kuhusu taasisi za kifedha za Kiislamu. Wasomi wa masuala ya kiuchumi nchini Iran na halikadhalika wataalamu 35 kutoka nchi zingine 10 watashiriki katika kikao hicho.