Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yamefunguliwa rasmi katika Msikiti wa Fatih, kati kati ya mji wa Istanbul.
Mashindano ya mwaka huu yatakuwa na washiriki 89 wasomaji (quraa) na waliohifadhi Qur'ani (hufadh) kutoka nchi 55.
Mashindano hayo huandaliwa na Idara ya Masuala ya Kidini ya Uturuki katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Wanaoandaa mashindano hayo wanasema lengo ni kustawisha utamaduni wa Qur'ani na kuhimiza usomaji na kuhifadhi Kitabu hicho Kitakatifu. Jopo la majaji katika mashindano ya mwaka hii ni wataalamu wa Qur'ani kutoka Uturuki, Malaysia, Saudi Arabia, Morocco, Lebanon na Somalia.
Mashindano hayo yanatazamiwa kuendelea hadi Juni 16 na washiriki watatunukiwa zawadi katika sherehe itakayofanyika Ijumaa Juni 17.