IQNA

Wafuasi wa dini zote wanaishi kwa amani Iran

10:20 - January 29, 2017
Habari ID: 3470818
IQNA: Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu daima katika kipindi chote cha histroia yake imekuwa ni yenye kufuatilia suala la kuweko amani na urafiki.

Rais Rouhani amesema hayo leo hapa mjini Tehran katika hotuba yake kwenye mkutano wa 17 wa Shirikisho la Kimattaifa la Jumuiya za Viongozi wa Misafara ya Utalii na kubainisha kwamba, nchini Iran kuna maisha ya amani baina ya wafuasi wa dini za Mwenyezi Mungu kando ya msikiti na kanisa na kwamba katika Bunge la Iran wafuasi wa dini za Uyahudi, Ukristo na Uzartoshti wana wawakilishi wao wakiwa pamoja na wawakilishi wa Waislamu katika Bunge hilo.

Rais wa Iran amesema, moja ya malengo makuu ya taifa lenye utamaduni na ustaarabu wa miaka elfu saba wa Iran katika Mashariki ya Kati na ulimwengu kwa ujumla ni kuweko mfungamano baina ya mataifa mbalimbali.

Rais Rouhani amesema kuwa, hizi si zama za mataifa kujengeana ukuta na kwamba hata kama kutakuweko ukuta baina ya mataifa, basi ukuta huo unapaswa kuvunjwa na hivyo kuondoa vizuizi baina ya mataifa.

Rais Hassan Rouhani sambamba na kutangaza utayari wa Iran wa kusaidia kupambana na ugaidi katika eneo lolote lile duniani amesema kuwa, kwa bahati nzuri hii leo ugaidi unaelekea kutokomea katika Mashariki ya Kati.

Kwingineko katika hotuba yake, Rais Rouhani amesema Iran imeshuhudia ongezeko kubwa la watalii tokea kutiwa saini mapatnao yake nyuklia baina yake na madola sita makubwa duniani mwaka 2015.

3567327
Kishikizo: hassan rouhani iqna
captcha