IQNA

Kuondoa vikwazo vya lugha: Tafsiri ya lugha 17 yazinduliwa katika maeneo matakatifu ya Uislamu

15:38 - May 17, 2026
Habari ID: 3482249
IQNA – Mamlaka zinazosimamia Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume mjini Madina zimeanza kutumia mfumo wa tafsiri ya papo kwa papo kwa lugha nyingi.

Urais wa Masuala ya Kidini katika Msikiti Mkuu wa Makka (Masjid Al Haram) na Msikiti wa Mtume (Al Masjid An Nabawi) umetangaza kuanzishwa kwa mfumo wa tafsiri ya papo hapo katika lugha 17 tofauti.

Mfumo huo unatumia teknolojia za kisasa za sauti, uchakataji wa maandishi na akili mnemba au AI ili kutoa tafsiri ya haraka ya maudhui ya mwongozo wa kidini pamoja na majibu ya maswali ya kifiqhi na kidini, kwa lengo la kurahisisha mawasiliano na mahujaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Mpango huu unaotegemea teknolojia ni sehemu ya juhudi za mabadiliko ya kidijitali zinazoendeshwa na urais huo ili kuboresha ubora wa huduma za kidini hasa katika kipindi cha msimu wa Hija.

Kwa kutumia teknolojia za kisasa, mpango huu unalenga kufikisha ujumbe wa Misikiti Miwili Mitukufu kwa hadhira ya kimataifa, na kuhakikisha kuwa wageni wa kimataifa wanaweza kupata kwa urahisi na kwa ufanisi huduma muhimu za mwongozo na uelimishaji wa kidini.

3497488

captcha