IQNA

13:03 - August 18, 2019
News ID: 3472090
TEHRAN (IQNA) – Polisi ya Norway imewashukuru wazee wawili Waislamu ambao walimshinda nguvu gaidi ambaye alikuwa analenga kuwaua Waislamu katika msikiti mmoja mjini Baerum.

Mohamed Rafiq, 25 na Mohamed Iqbal Jave 70, walimzuia gaidi Philip Manshaus kuwafyatulia risasi waumini waliokuwa wamefika katika Masjdi al Noor Agosti 10 magharibi mwa mji mkuu Oslo.

Lisbeth Hammer Krog Meya wa Baerum pamoja na mkuu wa polisi mjini wamewakaribisha Waislamu hao kwa shada la maua walipotembelea makao makuu ya polisi.

Mkuu wa Polisi Baerum Beat Gangas Krog amewashukuru Waislamu hao kwa ushujaa wao ambao uliokoa maisha ya idadi kubwa ya watu.

Kwa mujibu wa taarifa, gaidi Philip Manshaus, 21, akiwa na bunduki alifika katika Masjid al Noor Agosti 10 kwa lengo la kuwaua Waislamu na alianza  kufyatua risasi karibu mlango wa nyuma wa msikiti. Hapo Rafiq na Jave walielekea alipokuwa amesimami na mushinda nguvu. Gaidi huyo mzungu mwenye misimamo ya kibaguzi na kujiona bora, alikuwa amemuua dada yake wa kambo, Johanne Zhangjia Ihle-Hansen, mwenye asili ya China, kabla ya kuelekea katika msikiti kwa lengo la kuwaua Waislamu.

Hivi sasa Manshaus yuko kizuizini na atafunguliwa mashtaka ya mauaji na ugaidi.

3469187/

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: