IQNA

14:56 - December 02, 2019
News ID: 3472251
TEHRAN (IQNA) – Adhana imesikika kwa mara ya kwanza katika msikiti mmoja mkongwe nchini kaskazini mwa Macedonia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 107.

Mnara wa Msikiti wa Ali Pasha katika mji wa Ohrid uliharibiwa katika Vita vya Balkan (1912-1913), vita ambavyo viliandaa mazingira vya Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia.

Mradi wa kuukarabati msikiti huo na mnara wake uligharimu dola milioni 2.5.

Sasa kwa mara kwa kwanza kabisa baada ya karne moja, Adhana imesikika tena katika msikiti huo.

Msikiti wa Ali Pasha ulijengwa mwka 1573 kwa amri ya watawala wa utawala wa Othmaniyya.

3860941

 

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: