IQNA

Kikosi cha PMU cha Iraq chaangamiza magaidi na kuzima hujuma

11:02 - December 20, 2020
Habari ID: 3473473
TEHRAN (IQNA) - Askari wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi Iraq (PMU) maarufu kama Hashdu Shaabi wamefanikiwa kuwaangamiza magaidi watano sambamba na kuzima hujuma ya kigaidi katika eneo la al-Oaista mjini Jurf al Nasr mkoani Babel, kusini mwa mji mkuu Baghdad.

Kamandi ya Opareseheni za Pamoja Iraq imeyasema hayo katika ripoti yake kuhusu oparesheni za usalama katika mikoa minne ya Iraq.

Kamandi hiyo imesema oparesheni mkoani Babel imetekelezwa na Brigedi ya 47 ya Hashdu Shaabi. Aidha taarifa hiyo imesema Jeshi la Iraq limefanikiwa kuwakamata magaidi wanne huko Kirkuk na Al Anbar. 

Imedokezwa kuwa katika oparesehni hiyo mabomu ya magaidi wa ISIS yamenaswa na kuharibiwa.

Hayo yanajiri wakati ambao Marekani inajaribu kutangaza kikosi cha Hashdu Shaabi, ambacho pia hujulikana kama Taasisi ya Badr, kuwa eti ni kundi la kigaidi. Wapiganaji wa Hashdu Shaabi wamekuwa na nafasi muhimu katika kuangamiza magaidi wa ISIS na kukomboa maeneo yaliyokuwa yametekwa na magaidi hao kote Iraq. Mwezi Novemba mwaka 2016 Bunge la Iraq liliidhinisha Hashdu Shaabi kujiunga na jeshi la nchi hiyo.

3473450

captcha