IQNA

Hizbullah: Hashdu Shaabi imepata medali ya fahari kuwekewa vikwazo na Marekani

19:05 - January 09, 2021
Habari ID: 3473541
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa na kusema hatua ya Marekani kuiwekea vikwazo Harakati ya Wapiganaji wa Kujitolea Iraq maarufu kama Al Hashd Al Shaabi (PMU( ni sawa na kuipa harakati hiyo medali ya fahari.

Ofisi ya udhibiti wa mali za kigeni ya wizara ya fedha ya Marekani ilitangaza Ijumaa usiku kuwa, jina la Falih al-Fayyaz, Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi ya Iraq limewekwa kwenye orodha ya vikwazo ya Washington.

Katika jibu ililotoa kwa hatua hiyo ya Marekani ya kumwekea vikwazo Falih al-Fayyaz, Harakati ya Hizbullah ya Lebanon leo imetoa taarifa na kueleza kwamba, vikwazo hivyo ni nyongeza ya mlolongo wa jinai zinazoendelea kufanywa na Marekani dhidi ya Iraq na watu wake.

Katika taarifa yake hiyo, Hizbullah imesema, sababu kuu ya Salih al-Fayyaz kuwekewa vikwazo na Marekani ni msimamo wake thabiti kuhusiana na uvamizi wa Marekani na kutokubali kuhalalisha uwepo wa wavamizi hao katika ardhi ya Iraq na vilevile nafasi ya Al-Hashdu-Sha'abi katika kupambana na magaidi wa DAESH (ISIS).

Kitambo si kirefu nyuma, Falih al-Fayyaz, Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi ya Iraq alitoa indhari kuhusu njama zinazofanywa kwa lengo la kuchafua jina la jeshi hilo la kujitolea la wananchi wa Iraq.

3946584

captcha