IQNA

Watu wa Basra waanza matembezi ya Arobaini ya Imam Hussein AS

TEHRAN (IQNA)- Wakaazi wa mji wa Basra kusini mwa Iraq wameanza matembezi ya kuelekea katika mji mtakatifu wa Karbala kushiriki katika Ziyara ya Arobaini ya Imam Hussein AS.

Kwa mujibu wa taarifa, wanaume, wanawake na hata watoto wameanza safari ya matembezi hayo ya Arobaini au Arbaeen. Kutokana na mji wao kuwa mbali wakaazi wa Basra huanza matembezi ya Arobaini mapema kwani watatembea kwa miguu masafa ya kilomita 520 kabla ya kufika Karbala katika Siku ya Arobaini.

Majlisi na  ya siku ya Arobaini hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria, baada ya kupita siku Arobaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram, kwa ajili ya kukumbuka siku aliyouawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbalamwaka 61 Hijria Qamaria. Haram Takatifu ya Imam Hussein AS iko katika mji huo wa Karbala.

Watu wa Iraq hutembea kwa miguu kutoka miji yao ya mbali na karibu ili kufika Karbala katika siku hiyo ya Arobaini. Halikadhalika wafanyaziara kutoka nchi mbali mbali hushiriki kwa mamilioni katika hafla hiyo. Mwaka huu kutokana na vizingiti vya corona idadi ya washiriki wa Arobaini inatazamiwa kupungua.

 Siku ya Arobaini ambayo mwaka huu intazamiwa kusadifiana na Septemba 27.

3995475

Kishikizo: arbobaini ، imam hussein as ، basra ، karbala