IQNA

Kongamano la Kimataifa la Arubaini lafanyika Karbala

22:42 - September 13, 2021
Habari ID: 3474291
TEHRAN (IQNA)- Awamu ya 5 ya Kongamano la Kimataifa la Arubaini ya Imam Hussein AS limefanyika kwa muda wa siku mbili mjini Karbala Iraq.

Kongamano hilo ambalo limefanyika katika Haram Takatifu ya Imam Hussein AS limejadili masuala ya vijana na hujuma za kiutamaduni wanazokabiliana nazo.

Washiriki wa kongamano hilo ambalo limefanyika Septemba 10 na 11 walikuwa ni kutoka nchi  kama vile Ufaransa, Saudi Arabia, Tunisia, Misri, Iran na Lebanon.

Kulikuwa na makala 120 zilizowasilishwa na wasomi ambapo mbali na mada ya vijana washiriki pia wamejadili masuala muhimu ya Siku ya Arubaini ya Imam Hussein AS kama vile masuala ya afya, uchumi, jamii na fedha.

Maadhimisho ya siku ya Arobaini (Arubaini au Arbaeen) hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria, baada ya kupita siku Arobaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram, kwa ajili ya kukumbuka siku aliyouawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbalamwaka 61 Hijria Qamaria. Haram Takatifu ya Imam Hussein AS iko katika mji huo wa Karbala.

Watu wa Iraq hutembea kwa miguu kutoka miji yao ya mbali na karibu ili kufika Karbala katika siku hiyo ya Arobaini. Halikadhalika wafanyaziara kutoka nchi mbali mbali hushiriki kwa mamilioni katika hafla hiyo. Mwaka huu kutokana na vizingiti vya corona idadi ya washiriki wa Arobaini inatazamiwa kupungua.

 Siku ya Arobaini ambayo mwaka huu intazamiwa kusadifiana na Septemba 27.

 

 

3996924

Kishikizo: arubaini ، imam hussein as ، karbala
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha